P-Square: Jinsi nyota maarufu wa Afrobeat walivyojikuta katika hali ya kutengena tena

Wakiwa mapacha walioimba pamoja P-Square, walitawala muziki wa Afrobeat nchini Nigeria kwa miaka mingi na walikuwa moja ya vikundi vya kwanza kueneza muzikii huo katika sehemu nyingine za bara. Kuvunjika kwa kundi hilo kati ya pacha Peter na Paul Okoye waliofahamika maarufu P-Square ni jambo linalokaribia kukamilika.

Malumbano ya pacha hao wa Nigeria ambayo yamechochewa na migogoro ya ndani, kwa sasa hayaonyeshi dalili ya kumalizika wakati wowote hivi karibuni.

Barua ya wazi iliyowekwa kwenye mitandao ya kijamii ya mmoja wa mapacha hao kufuatia madai ya makosa ya kifedha yanayomhusisha mmoja wa pacha hao, imeonyesha kuongezeka kwa uhasama baina yao.

Own handsome delicate its property mistress her end appetite

Katika chapisho kwenye Instagram na Facebook Jumatatu, Agosti 12, 2024, Peter “Mr. P” Okoye alielezea kusikitishwa kwake na wasiwasi wake juu ya msururu wa taarifa za umma za hivi karibuni za kaka yake, Paul “Rudeboy” Okoye, ambazo alisema zimepotosha ukweli kuhusu kazi yao kwa pamoja na michango yake ya kibinafsi kwa kundi hilo.

Petro anamtuhumu kaka yake pacha, Paulo kwa kuharibu urithi wa bendi ambayo wote wawili waliijenga pamoja.

“Kwa kaka yangu mpendwa Paul Okoye aka Rudeboy, kama ambavyo nimekua nikikuambia mara nyingi, siko katika ushindani na wewe au mtu mwingine yeyote.

Hata hivyo, kukuona unaposhiriki mahojiano mengi ukionyesha kudharau juhudi zangu katika kundi ambalo sisi wote tumeliunda na kulijenga pamoja ina maana kubwa.

Post navigation

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ikiwa unapenda chapisho hili unaweza kupenda haya

error: Content is protected !!