Idris Elba: Kwa nini ninapanga kuhamia Afrika?

Mwigizaji wa Uingereza Idris Elba ameiambia BBC kwamba atahamia Afrika ndani ya muongo mmoja ujao, ikiwa ni sehemu ya mipango yake ya kusaidia tasnia ya filamu barani humo.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 52, ana mpango wa kujenga studio ya filamu katika visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania, na studio nyingine katika mji mkuu wa Ghana, Accra.


Mzaliwa wa London, Elba, ambaye mama yake anatoka Ghana na baba yake anatokea Sierra Leone, ana uhusiano mkubwa na Afrika.

Savvy Media

Anataka kutumia uwezo wake ili kuunga mkono biashara ya filamu inayoendelea kukua – kwani anasema ni muhimu Waafrika wapate kusimulia hadithi zao wenyewe.

“Kwa hakika nafikiria kuhamia hapa; sio kufikiria, nitahamia,” alisema katika mahojiano kando ya mkutano wa tasnia ya filamu huko Accra.

“Nafikiri [nitahamia] katika miaka mitano ijayo, au 10, Mungu akipenda. Niko hapa ili kukuza tasnia ya filamu – huo ni mchakato wa miaka 10 – sitaweza kufanya hivyo nikiwa ng’ambo. Napaswa kuwa ndani ya nchi, ndani ya bara.”

Post navigation

Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Ikiwa unapenda chapisho hili unaweza kupenda haya

error: Content is protected !!